Surat Al-Anfal, aya 71

8:71

وَإِن يُرِيدُواْ خِيَانَتَكَ فَقَدۡ خَانُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ فَأَمۡكَنَ مِنۡهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ٧١

Wa in yurīdū khiyānataka faqad khānullāha min qablu fa amkana minhum wallāhu 'alīmun hakīm

Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana Mwenyezi Mungu kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. 71

Maelezo ya chini

71 Na pindi wakitaka kukukhuni, kwa vile baadhi yao walivyo onyesha kumili kwenye Uislamu, pamoja na nyoyo zao kupenda kukufanyia khiana makusudi, wewe usivunjike moyo. Mwenyezi Mungu atakupa uwezo juu yao. Kama hapo kwanza walipo mkhini Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia wenzi na washirika wa kuwaabudu, na wakaikufuru neema yake, na Yeye aliwaweza kwa kukupa ushindi juu yao katika Badri, juu ya kuwa jeshi lako ni dogo na lao ni kubwa. Na Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye ushindi, Muendeshaji kwa hikima yake, aliwathibitisha wakawa na nguvu waja wake Waumini kwa nusura yake.