Surat Al-Anfal, aya 49

8:49

إِذۡ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمۡۗ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٞ ٤٩

Idh yaqūlul-munāfiqūna walladhīna fī qulūbihim maradun gharra hā'ulā'i dīnuhum waman yatawakkal 'alallāhi fa innallāha 'azīzun hakīm

Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima. 49

Maelezo ya chini

49 Na kumbuka ewe Mtume! Walipo sema wanaafiki miongoni mwa makafiri na wale wenye Imani dhaifu walipo kuoneni mmesimama imara: Hawa Waislamu wameghurika kweli na dini yao! Na hakika mwenye kumwakilisha Mwenyezi Mungu jambo lake, na akamuamini Yeye, na akamtegemea Yeye, basi hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu atamkifia amwondolee hamu yake, na atamnusuru na maadui zake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu madaraka yake yana nguvu, naye ni Mwenye hikima katika mipango yake.