يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمۡ فِئَةٗ فَٱثۡبُتُواْ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ ٤٥
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū idhā laqītum fi atan fathbutū wadhkurullāha kathīral la'allakum tuflihūn
Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa. 45
Maelezo ya chini
45 Enyi mlio amini! Mkikutana na kikosi cha wapiganaji katika adui zenu, basi kuweni imara, wala msiwakimbie. Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa kufuata uwezo wake, na ahadi yake ya kuwasaidia Waumini, mkikithirisha kumkumbuka na kumtaja pamoja na kuwa imara na kusubiri. Mkifanya hivyo ndio matarajio yenu ya kupata mafanikio yatapo timia.