إِذۡ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى ٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ أَنِّي مَعَكُمۡ فَثَبِّتُواْ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْۚ سَأُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ فَٱضۡرِبُواْ فَوۡقَ ٱلۡأَعۡنَاقِ وَٱضۡرِبُواْ مِنۡهُمۡ كُلَّ بَنَانٖ ١٢
Idh yūhī rabbuka ilal-malā'ikati annī ma'akum fathabbitul-ladhīna āmanū sa'ulqī fī qulūbil-ladhīna kafarur-ru'ba fadribū fawqal-a'nāqi wadribū minhum kulla banān
Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole. 12
Maelezo ya chini
12 Enyi Waumini! Kumbukeni pale Mwenyezi Mungu alipo wafunulia wale wenye Roho zilio t'ahirika, yaani Malaika, watie ndani ya nyoyo zenu kuwa Mimi ni pamoja nanyi, nakuungeni mkono, na ninakusaidieni, kwa kuwaambia: Zitieni nguvu nyoyo za walio amini, wait'ii Haki na wapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mimi nitaifanya khofu izitawale nyoyo za washirikina, nao watakuogopeni. Nanyi enyi Waumini! Wapigeni vichwani mwao vilio juu ya shingo zao, na kateni vidole vyao vinavyo kamata panga.