Surat Al-Anfal, aya 13

8:13

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ شَآقُّواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ وَمَن يُشَاقِقِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ١٣

Dhālika bi annahum shāqqullāha warasūlahū waman yushāqiqillāha warasūlahū fa innallāha shadīdul-'iqāb

Hayo ni kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 13

Maelezo ya chini

13 Ukawa ushindi na kuungwa mkono nyinyi, na kwao ni kitisho na fazaa, kwani wao walikuwa upande mmoja, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake walikuwa upande mwengine, kwa kuwa wao walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi ndio Mwenyezi Mungu anawateremshia adhabu chungu. Na adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.