وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ كُلًّا هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَٰرُونَۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٨٤
Wawahabnā lahū ishāqa waya'qūba kullan hadaynā wanūhan hadaynā min qablu wamin dhurriyyatihī dāwūda wasulaymāna wa ayyūba wayūsufa wamūsā wahārūna wakadhālika najzil-muhsinīn
Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. 84
Maelezo ya chini
84 Na Sisi tulimpa Ibrahim, Is-haq na Yaaqub bin Is-haq. Na tukamwezesha kila mmoja wao kufikia Haki na Kheri, kama baba yao. Na kabla yake tulimwezesha Nuhu hivyo hivyo, na tukawaongoa katika wazao wa Nuhu, Daud, na Suleiman, na Ayyub, na Yusuf, na Musa, na Harun. Kama tulivyo walipa hawa, tunawalipa wafanyao wema kwa wanavyo stahiki.