Surat Al-An'am, aya 83

6:83

وَتِلۡكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيۡنَٰهَآ إِبۡرَٰهِيمَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ ٨٣

Watilka hujjatunā ātaynāhā ibrāhīma 'alā qawmihī narfa'u darajātim man nashā'u inna rabbaka hakīmun 'alīm

Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi. 83

Maelezo ya chini

83 Na hiyo hoja kubwa ya Ungu wetu, na Umoja wetu, tulimpa Ibrahim aisimamishe kupambana na watu wake, naye kwa hiyo akatukuka juu yao. Na mtindo wetu kwa waja wetu ni kuwa tunamnyanyua madaraja kwa ujuzi na hikima tumpendaye katika wao. Hakika Mola Mlezi wako, ewe Nabii, ni Mwenye hikima. Huweka kila kitu pahala pake. Ni Mwenye kuwajua wepi wanastahiki kutukuzwa, na wepi hawastahiki.