بَلۡ بَدَا لَهُم مَّا كَانُواْ يُخۡفُونَ مِن قَبۡلُۖ وَلَوۡ رُدُّواْ لَعَادُواْ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ٢٨
Bal badā lahum mā kānū yukhfūna min qablu walaw ruddū la'ādū limā nuhū 'anhu wa innahum lakādhibūn
Bali yamewadhihirikia waliyo kuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangeli rudishwa bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyo katazwa. Na hakika hao ni waongo. 28
Maelezo ya chini
28 Na kauli yao hii haikuwa ila kwa kuwa haimkiniki tena kuficha wala kufanya ukaidi katika yale anayo waambia Mtume. Na lau kama wakirudishwa duniani wataurejea tena ukafiri alio wakataza Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa ghururi zao kughurika na mapambo ya dunia, na kwa kufuata kwao matamanio yao. Na hakika hao wanasema uwongo kwa kudai kuwa wataamini pindi wakirejeshwa duniani.