وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُواْ يَٰلَيۡتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٢٧
Walaw tarā idh wuqifū 'alan-nāri faqālū yālaytanā nuraddu walā nukaddhiba bi'āyāti rabbinā wanakūna minal-mu'minīn
Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini. 27
Maelezo ya chini
27 Ewe Nabii! Lau ungeli waona hawa makafiri, watavyo simama mbele ya Moto wakisononeka na vitisho vyake, ungeli ona jambo la ajabu lenye kutisha, nao wanatamani warejeshwe tena duniani, wakisema: Laiti tungeli rudishwa duniani tukatengeneza tuliyo yaharibu! Wala hatutakanusha Ishara za Mola wetu Mlezi. Na tutakuwa miongoni wa Waumini.