Surat Al-An'am, aya 143

6:143

ثَمَٰنِيَةَ أَزۡوَٰجٖۖ مِّنَ ٱلضَّأۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡمَعۡزِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ نَبِّـُٔونِي بِعِلۡمٍ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ١٤٣

Thamāniyata azwājim minad-da'nithnayni waminal-ma'zithnayni qul āddhakarayni harrama amil-unthayayni ammashtamalat 'alayhi arhāmul-unthayayni nabbi'ūnī bi'ilmin in kuntum sādiqīn

Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli. 143

Maelezo ya chini

143 Mwenyezi Mungu ameumba katika kila namna ya nyama hoa dume na jike. Hizo basi ni namna nane. Kondoo namna mbili, mbuzi namna mbili. (ngamia na ng'ombe wametajwa katika Aya inayo fuata.) Ewe Muhammad! Waambie washirikina kukanya hayo waliyo yaharimisha: Nini sababu ya kuharimisha katika hawa kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa madume? Au kwa kuwa ni kuwa matumboni ya mama zao? Hayo hayawezi kuwa hivyo, kwa sababu nyinyi hamkuharimisha watoto waliomo tumboni kabisa!! Nambieni kwa mategemeo baraabara, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika kuhalalisha na kuharimisha.