وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ ١٤٢
Waminal-an'āmi hamūlatan wafarshan kulū mimmā razaqakumullāhu walā tattabi'ū khutuwātish-shaytāni innahū lakum 'aduwwum mubīn
Na katika wanyama amekujaalieni wenye kubeba mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu dhaahiri. 142
Maelezo ya chini
142 Na Mwenyezi Mungu ameumba katika nyama hoa, nao ni ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, wale wanao beba mizigo yenu, na wale ambao katika sufi yao na manyoya yao na nyewele zao mnatoa matandiko. Na hiyo ni riziki aliyo kujaalieni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni alicho kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msimfuate Shetani na marafiki zake katika kuzua vya halali na haramu, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa Jahiliya! Hakika Shetani hakutakiini kheri, kwa sababu yeye ni adui yenu, mwenye uadui dhaahiri.