Surat Al-An'am, aya 144

6:144

وَمِنَ ٱلۡإِبِلِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ وَصَّىٰكُمُ ٱللَّهُ بِهَٰذَاۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا لِّيُضِلَّ ٱلنَّاسَ بِغَيۡرِ عِلۡمٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٤٤

Waminal-ibilithnayni waminal-baqarithnayni qul āddhakarayni harrama amil-unthayayni ammashtamalat 'alayhi arhāmul-unthayayni am kuntum shuhadā'a idh wassākumullāhu bihādhā faman azlamu mimmaniftarā 'alallāhi kadhibal liyudillan-nāsa bighayri 'ilmin innallāha lā yahdil-qawmaz-zālimīn

.Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu. 144

Maelezo ya chini

144 Na Mwenyezi Mungu ameumba ngamia namna mbili, dume na jike, na ng'ombe namna mbili mbili vile vile. Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanya: Nini sababu ya kuwaharimisha hao mlio harimisha kama mnavyo dai? Ni kwa kuwa wao ni madume? Sivyo hivyo; kwa sababu pengine mnahalalisha madume! Au ni kwa kuwa majike? Pia sio hivyo, kwa sababu mnahalalisha majike wakati mwingine! Au kwa kuwa wana watoto matumboni mwao? Pia sio hivyo, kwa sababu hamkuharimisha watoto walio matumboni daima. Nanyi mnadai kuwa kuharimisha huku kunatokana na Mwenyezi Mungu! Nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuharimisheni haya na mkamsikia makatazo yake? Kabisa hayo hayakuwa. Wacheni mlio nayo; kwani hiyo ni dhulma. Na hapana mwenye kudhulumu zaidi kuliko mwenye kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, akamnasibisha nayo mambo yasiyo toka kwake, wala hayana tegemeo lolote la ki-ilimu la kutegemea, bali huyo anataka kuwapotosha watu tu! Mwenyezi Mungu hawawafikishi wenye kudhulumu wakikhiari njia ya upotovu.