قُلۡ يَٰقَوۡمِ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنِّي عَامِلٞۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَٰقِبَةُ ٱلدَّارِۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ ١٣٥
Qul yāqawmi'malū 'alā makānatikum innī 'āmilun fasawfa ta'lamūna man takūnu lahū 'āqibatud-dāri innahū lā yuflihuz-zālimūn
Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na hakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa. 135
Maelezo ya chini
135 Ewe Nabii! Waambie kwa kuwatisha: Fanyeni kama mpendavyo kwa ukomo wa uwezo wenu. Na mimi nitafanya kwa mujibu wa Haki. Na mwishoe bila ya shaka mtajua nani atakuwa na khatima njema katika makaazi ya Akhera. Na hayo watayapata watu wa Haki, hapana hivi wala hivi. Kwa sababu nyinyi ni madhaalimu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuwaandikia kufuzu walio dhulumu.