إِنَّ مَا تُوعَدُونَ لَأٓتٖۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعۡجِزِينَ ١٣٤
Inna mā tū'adūna la'ātin wamā antum bimu'jizīn
Bila ya shaka hayo mnayo ahidiwa yatafika tu, wala nyinyi hamtaweza kuyaepuka. 134
Maelezo ya chini
134 Na hayo anayo kuonyeni kwayo, nayo ni adhabu, na anayo kubashirieni kwayo, nayo ni thawabu baada ya kufufuliwa, na kukusanywa, na kuhisabiwa, yatakuja tu hapana hivi wala hivi. Wala nyinyi hamwezi kumshinda huyo anaye kutakeni Siku hiyo. Basi hamna uwezo wa kukataa kukusanyika wala kuhisabiwa.