Surat Al-Ahzab, aya 43

33:43

هُوَ ٱلَّذِي يُصَلِّي عَلَيۡكُمۡ وَمَلَٰٓئِكَتُهُۥ لِيُخۡرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَكَانَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَحِيمٗا ٤٣

Huwal-ladhī yusallī 'alaykum wamalā'ikatuhū liyukhrijakum minaz-zulumāti ilan-nūri wakāna bil-mu'minīna rahīmā

Yeye na Malaika wake ndio wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini. 43

Maelezo ya chini

43 Na Yeye ndiye aliye kuahidini kukupeni rehema yake na upole wake. Na Malaika wake wanakuombeeni maghfira na uwongofu, ili Mwenyezi Mungu akutoeni kwenye giza la ukafiri na upotovu, mwendee kwenye nuru na ut'iifu. Na Mwenyezi Mungu hakika ni Mkuu wa kuwarehemu Waumini.