وَإِذۡ قَالَت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ يَٰٓأَهۡلَ يَثۡرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمۡ فَٱرۡجِعُواْۚ وَيَسۡتَـٔۡذِنُ فَرِيقٞ مِّنۡهُمُ ٱلنَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوۡرَةٞ وَمَا هِيَ بِعَوۡرَةٍۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارٗا ١٣
Wa idh qālat tā'ifatum minhum yā'ahla yathriba lā muqāma lakum farji'ū wayasta'dhinu farīqum minhumun-nabiyya yaqūlūna inna buyūtanā 'awratun wamā hiya bi'awratin in yurīdūna illā firārā
Na kundi moja katika miongoni mwao lilipo sema: Enyi watu wa Yathrib! Hapana kukaa nyinyi! Rudini. Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa tupu; hawakutaka ila kukimbia tu. 13
Maelezo ya chini
13 Na kumbuka walipo sema kikundi cha wanaafiki na ambao wanao rega rega: Enyi watu wa (Yathrib, yaani) Madina! Hapana maana kubakia hapa nyinyi katika vita hivi vya kushindwa. Rudini mwende makwenu. Na kundi jingine kati yao walimtaka ruhusa Mtume warejee Madina, na wakasema: Hakika nyumba zetu hazina ulinzi. Hatuna budi kurejea tukazilinde. Wala nyumba zao hazikuwa khatarini kabisa kama walivyo sema. Hawakutaka ila kukimbia vita tu, kwa udhuru wa uwongo.