ٱذۡهَبُواْ بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلۡقُوهُ عَلَىٰ وَجۡهِ أَبِي يَأۡتِ بَصِيرٗا وَأۡتُونِي بِأَهۡلِكُمۡ أَجۡمَعِينَ ٩٣
Idhhabū biqamīsī hādhā fa alqūhu 'alā wajhi abī ya'ti basīran wa tūnī bi ahlikum ajma'īn
Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona. Na mje nao watu wenu wote wa nyumbani. 93
Maelezo ya chini
93 Kisha Yusuf akawauliza khabari za baba yao. Walipo mwambia kuwa hali yake ni mbaya na hawezi kuona kwa wingi wa hamu na majonzi, aliwapa kanzu yake, na akawaambia: Rejeeni kwa baba yangu, na hii kanzu mwekeeni usoni pake. Kwa hivyo atakuwa na yakini kuwa mimi nimo katika salama, na moyo wake utajaa furaha, na Mwenyezi Mungu atamjaalia iwe ni sababa ya kurejea kuona kwake. Hapo tena njooni naye kwangu, na ahali zenu wote pamoja.