قَالَ لَا تَثۡرِيبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَۖ يَغۡفِرُ ٱللَّهُ لَكُمۡۖ وَهُوَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ ٩٢
Qāla lā tathrība 'alaykumul-yawma yaghfirullāhu lakum wahuwa arhamur-rāhimīn
Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu. 92
Maelezo ya chini
92 Yule Nabii mtukufu akawajibu kwa kusema: Hapana lawama kwenu leo, wala kusutana. Lenu kutoka kwangu ni msamaha ulio mwema kwa fadhila ya nasaba na haki ya udugu. Na namuomba Mwenyezi Mungu akusameheni na akughufirieni. Na Yeye ndiye Mwenye rehema kuu.