Surat Yusuf, aya 94

12:94

وَلَمَّا فَصَلَتِ ٱلۡعِيرُ قَالَ أَبُوهُمۡ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَۖ لَوۡلَآ أَن تُفَنِّدُونِ ٩٤

Walammā fasalatil-'īru qāla abūhum innī la ajidu rīha yūsufa lawlā an tufannidūn

Na ulipo ondoka tu msafara baba yao alisema: Hakika mimi nasikia harufu ya Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu 94

Maelezo ya chini

94 Wakaondoka na ile kanzu. Na moyo wa Yaa'qub ulikuwa umezama kungojea nini litalo leta safari ya wanawe. Na Mwenyezi Mungu alikuwa yu pamoja naye katika kungojea huko, ikawa roho yake imeshikamana na roho zao. Basi ule msafara wao ulipo toka nchi ya Misri katika njia yake kumwendea yeye, aliwaambia ahali zake hayo kwa kusema: Mimi naihisi harufu ninayo ipenda ya Yusuf inanijaa. Na lau kuwa sikhofu kwamba mtanituhumu kwa niyasemayo ningeli kwambieni mengi ya Yusuf kuliko hizi hisiya na mawazo.