Surat Yusuf, aya 90

12:90

قَالُوٓاْ أَءِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُۖ قَالَ أَنَا۠ يُوسُفُ وَهَٰذَآ أَخِيۖ قَدۡ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَآۖ إِنَّهُۥ مَن يَتَّقِ وَيَصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٩٠

Qālū a'innaka la anta yūsufu qāla ana yūsufu wahādhā akhī qad mannallāhu 'alaynā innahū man yattaqi wayasbir fa innallāha lā yudī'u ajral-muhsinīn

Wakasema: Kumbe wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anaye mcha Mungu na akasubiri, basi Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa wafanyao mema. 90

Maelezo ya chini

90 Kuzinduliwa huku kwa furaha kuliwatambulisha kwamba huyu ndiye Yusuf. Wakamtazama kisha wakasema kwa yakini: Hakika wewe ndiye kweli Yusuf! Na Yusuf mwenye ukarimu aliwaambia kwa kuwakubalia: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu yangu. Mwenyezi Mungu ametufadhili kwa kutuvua kwa salama tusihiliki, na kwa kutupa hadhi na madaraka! Na hayo yamekuwa ni malipo ya Mwenyezi Mungu kwa usafi wangu na wema wangu. Na hakika Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa mtendaji mema na akaendelea nao.