Surat Yusuf, aya 26

12:26

قَالَ هِيَ رَٰوَدَتۡنِي عَن نَّفۡسِيۚ وَشَهِدَ شَاهِدٞ مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن كَانَ قَمِيصُهُۥ قُدَّ مِن قُبُلٖ فَصَدَقَتۡ وَهُوَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ٢٦

Qāla hiya rāwadatnī 'an nafsī washahida shāhidum min ahlihā in kāna qamīsuhū qudda min qubulin fasadaqat wahuwa minal-kādhibīn

Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliye kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo. 26

Maelezo ya chini

26 Yusuf akasema kujitetea: Ni yeye ndiye aliyenitaka, na akajaribu kunikhadaa! Ikawa ni kusutana. Alikata hukumu mmojapo katika jamaa zake mwenyewe yule mwanamke kwa kusema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele, basi huyu bibi kasema kweli katika madai yake, na huyu kijana ni mwongo kwa aliyo yasema.