Surat Yusuf, aya 110

12:110

حَتَّىٰٓ إِذَا ٱسۡتَيۡـَٔسَ ٱلرُّسُلُ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ كُذِبُواْ جَآءَهُمۡ نَصۡرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَآءُۖ وَلَا يُرَدُّ بَأۡسُنَا عَنِ ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ١١٠

Hattā idhastay'asar-rusulu wazannū annahum qad kudhibū jā'ahum nasrunā fanujjiya man nashā'u walā yuraddu ba sunā 'anil-qawmil-mujrimīn

Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu. 110

Maelezo ya chini

110 Ewe Muhammad! Wala usione nusura yangu inakawia, kwani nusura yangu ipo karibu na hakika inakuja. Na Sisi tuliwatuma kabla yako Mitume, na kwa mujibu wa hikima yetu msaada wetu ulikawilia. Na wao wakawa wanaendelea kukanywa na watu wao, mpaka nafsi zilipo tikisika, wakahisi kukata tamaa, nusura yetu ikawadiriki; tukawaneemesha kwa kuwaokoa na kuwaletea amani wale walio stahili kutaka uwokofu kwetu, nao ni Waumini. Tukawageuzia maovu wale walio tenda dhambi kwa inadi na wakashikilia ushirikina. Wala hapana awezae kuizuia adhabu yetu isiwafikie watu wakosefu.