أَلَآ إِنَّ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهِ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ٦٢
Alā inna awliyā'allāhi lā khawfun 'alayhim walā hum yahzanūn
Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. 62
Maelezo ya chini
62 Enyi watu! Tanabahini na mjue ya kuwa wenye kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa Imani na ut'iifu Yeye anawapenda, na wao wanampenda. Hawana khofu ya kuhizika duniani, wala kupata adhabu ya Akhera. Wala wao hawahuzuniki kwa kukosa starehe za duniani, kwa kuwa watapata kwa Mwenyezi Mungu yaliyo makubwa na mengi kuliko hayo.