Surat Yunus, aya 57

10:57

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَشِفَآءٞ لِّمَا فِي ٱلصُّدُورِ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ ٥٧

Yā'ayyuhan-nāsu qad jā'atkum maw'izatum mir rabbikum washifā'ul limā fis-sudūri wahudan warahmatul lil-mu'minīn

Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini. 57

Maelezo ya chini

57 Enyi watu! Kimekujieni kwa ulimi wa Mtume Muhammad Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu. Ndani yake mna makumbusho ya Imani, na ut'iifu, na mawaidha ya kuhimiza kheri, na kukataza vitendo viovu, na kueleza mzingatie khabari za walio kutangulieni, na kukutakeni muangalie utukufu wa uumbaji ili mpate kuuelewa utukufu wa Muumba. Na ndani ya Kitabu hicho mna dawa ya maradhi ya nyoyo zenu, maradhi ya shirki na unaafiki; na mna uwongofu wa kuendea Njia Iliyo Nyooka. Na yote hayo ni rehema kwa Waumini wanao itikia wito.