Surat Yunus, aya 49

10:49

قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي ضَرّٗا وَلَا نَفۡعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ فَلَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ ٤٩

Qul lā amliku linafsī darran walā naf'an illā mā shā'allāhu likulli ummatin ajalun idhā jā'a ajaluhum falā yasta'khirūna sā'atan walā yastaqdimūn

Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja wala hawatangulii. 49

Maelezo ya chini

49 Ewe Mtume! Waambie: Mimi sina uwezo wa kujitendea mwenyewe kheri wala shari, ila kwa aliyo niwezesha Mwenyezi Mungu. Basi vipi niweze kuihimiza ije upesi hiyo adhabu? Hakika kila umma una ukomo wake aliyo uwekea Mwenyezi Mungu tangu na tangu. Ukiwadia ukomo huo basi hawatoweza kuuchelewesha hata kidogo, kama wasivyo weza kuutanguliza!