قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُهُۥ بَيَٰتًا أَوۡ نَهَارٗا مَّاذَا يَسۡتَعۡجِلُ مِنۡهُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ ٥٠
Qul ara'aytum in atākum 'adhābuhū bayātan aw nahāram mādhā yasta'jilu minhul-mujrimūn
Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya adhabu wanaihimiza wakosefu? 50
Maelezo ya chini
50 Waambie wanao himiza ifike adhabu: Hebu niambieni, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu usiku au mchana, pana faida gani watayo ipata wakosefu wenye madhambi kutaka ije kwa haraka? Na hali adhabu yote ni mbaya!