وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ كَأَن لَّمۡ يَلۡبَثُوٓاْ إِلَّا سَاعَةٗ مِّنَ ٱلنَّهَارِ يَتَعَارَفُونَ بَيۡنَهُمۡۚ قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ ٤٥
Wayawma yahshuruhum ka al lam yalbathū illā sā'atam minan-nahāri yata'ārafūna baynahum qad khasiral-ladhīna kaddhabū biliqā'illāhi wamā kānū muhtadīn
Na Siku atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya mchana! Watatambuana. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka. 45
Maelezo ya chini
45 Ewe Mtume! Wahadharishe na Siku tutayo wakusanya kwa ajili ya Hisabu, wawe na hakika kuwa Siku ya Akhera itakuja, baada ya kuwa walikuwa wakiikanusha na wakikumbuka maisha yao ya duniani tu. Waone ni kama saa moja tu ya mchana, hapana wasaa wa kufanya kitendo chochote cha kheri, na wajuane wao kwa wao wakilaumiana kwa kufuru na upotovu walio kuwa nao! Wamekhasiri wakanushao Siku ya Akhera na wasitangulize vitendo vyema katika dunia yao, na wakakosa neema za Akhera kwa kufuru zao.