Surat Yunus, aya 27

10:27

وَٱلَّذِينَ كَسَبُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ جَزَآءُ سَيِّئَةِۭ بِمِثۡلِهَا وَتَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ مَّا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنۡ عَاصِمٖۖ كَأَنَّمَآ أُغۡشِيَتۡ وُجُوهُهُمۡ قِطَعٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مُظۡلِمًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ٢٧

Walladhīna kasabus-sayyi'āti jazā'u sayyi'ati bimithlihā watarhaquhum dhillatum mā lahum minallāhi min 'āsimin ka annamā ughshiyat wujūhuhum qita'am minal-layli muzliman ulā'ika ashābun-nāri hum fīhā khālidūn

Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu. 27

Maelezo ya chini

27 Na wale ambao hawakuitikia Wito wa Mwenyezi Mungu, wakakufuru, wakatenda maasi, watalipwa kwa mujibu ya uovu walio utenda. Na hawana mlinzi wa kuwakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na nyuso zao zitasawajika kwa ghamu na huzuni kama kwamba zimefunikwa na weusi wa kiza cha usiku! Na hao ndio watu wa Motoni, watasononeka humo milele.