Surat Yunus, aya 28

10:28

وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ مَكَانَكُمۡ أَنتُمۡ وَشُرَكَآؤُكُمۡۚ فَزَيَّلۡنَا بَيۡنَهُمۡۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمۡ إِيَّانَا تَعۡبُدُونَ ٢٨

Wayawma nahshuruhum jamī'an thumma naqūlu lilladhīna ashrakū makānakum antum washurakā'ukum fazayyalnā baynahum waqāla shurakā'uhum mā kuntum iyyānā ta'budūn

Na siku tutakapo wakusanya wote, kisha tutawaambia walio shirikisha:Simameni mahali penu nyinyi na wale mlio wafanya washirika. Kisha tutawatenga baina yao. Na hao walio washirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi. 28

Maelezo ya chini

28 Ewe Mtume! Kumbuka kitisho cha siku watapo kusanywa viumbe vyote, kisha tuwaambie walio mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada zao: Simameni pahala penu nyinyi na hao mlio wafanya washirika wa Mwenyezi Mungu, muangalie mtafanywa nini? Patatokea mfarakano baina ya washirikina na hao miungu yao ya uwongo walio washirikisha na Mwenyezi Mungu. Hao miungu watajitenga na wale wafwasi wao, kwa kusema: Sisi hatukukutakeni mtuabudu. Wala nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi! Hakika mlikuwa mkiyaabudu matamanio yenu tu!