Surat Yunus, aya 26

10:26

۞ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ ٱلۡحُسۡنَىٰ وَزِيَادَةٞۖ وَلَا يَرۡهَقُ وُجُوهَهُمۡ قَتَرٞ وَلَا ذِلَّةٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ٢٦

Llilladhīna ahsanul-husnā waziyādatun walā yarhaqu wujūhahum qatarun walā dhillatun ulā'ika ashābul-jannati hum fīhā khālidūn

Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu. 26

Maelezo ya chini

26 Wanao tenda mema kwa kuitikia Wito wa Mwenyezi Mungu, wakaamini na wakafanya kheri kwa Dini yao na dunia yao, hao watapata wema katika Akhera, na wema huo ni Pepo. Na tena watapata yaliyo zidi hayo kwa fadhila na ukarimu wa Mwenyezi Mungu. Wala nyuso zao hazitafunikwa na huzuni na hamu na fedheha. Hawa ndio watu wa Peponi watakao neemeka humo daima milele.