Surat Yunus, aya 104

10:104

قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٠٤

Qul yā'ayyuhan-nāsu in kuntum fī shakkim min dīnī falā a'budul-ladhīna ta'budūna min dūnillāhi walākin a'budullāhal-ladhī yatawaffākum wa umirtu an akūna minal-mu'minīn

Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini. 104

Maelezo ya chini

104 Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa mna shaka na ukweli wa Dini niliyo tumwa kuileta kwenu, basi jueni kuwa kama mtavyo tia shaka mimi kabisa sitoabudu hayo masanamu mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu ambaye mambo yenu yote yapo mikononi mwake. Yeye ndiye anaye kutoeni roho. Na Yeye ameniamrisha niwe katika wanao muamini Yeye.