Surat Yunus, aya 10

10:10

دَعۡوَىٰهُمۡ فِيهَا سُبۡحَٰنَكَ ٱللَّهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمۡ فِيهَا سَلَٰمٞۚ وَءَاخِرُ دَعۡوَىٰهُمۡ أَنِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٠

Da'wāhum fīhā subhānakallāhumma watahiyyatuhum fīhā salāmun wa ākhiru da'wāhum anil-hamdu lillāhi rabbil-'ālamīn

Wito wao humo utakuwa: Subhanaka Llahumma "Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!" Na maamkio yao humo ni "Salama". Na mwisho wa wito wao ni: Alhamdulillahi Rabbil A'lamiin "Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote." 10

Maelezo ya chini

10 Dua za Waumini katika Bustani hizo ni kumsabihi na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila waliyo kuwa wakiyasema makafiri duniani, na kusalimiwa na Mwenyezi Mungu, na kusalimiana wao kwa wao ili kuthibitisha amani na utulivu. Na kukhitimishia dua yao ni kumhimidi Mwenyezi Mungu kwa tawfiqi yake, kuwawezesha, kufikia Imani na kufuzu kwao kuipata radhi yake.