Surat Yunus, aya 11

10:11

۞ وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ ١١

Walaw yu'ajjilullāhu lin-nāsish-sharrasti'jālahum bil-khayri laqudiya ilayhim ajaluhum fanadharul-ladhīna lā yarjūna liqā'anā fī tughyānihim ya'mahūn

Na lau kama Mwenyezi Mungu angeli wafanyia watu haraka kuwaletea shari kama wanavyo jihimizia kuletewa kheri, bila ya shaka wangelisha timiziwa ajali yao. Lakini tunawaacha wale wasio tumainia kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao. 11

Maelezo ya chini

11 Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli waitikia watu wanapo jiapizia shari kama vile wanavyo jihimizia kuitaka kheri, angeli waangamiza akawateketeza wote. Lakini Yeye anawachukulia kwa upole basi anaakhirisha kuwateketeza, ili kungojea wadhihirishe walio nayo kwa mujibu wa anavyo wajuulia, upate kuonekana wazi uadilifu wake kwa atavyo walipa. Wanaachwa na ushahidi wa kutosha umesimama dhidi yao, nao makusudi wanakengeuka na kuelekea njia ya upotovu na udhalimu.