Wa man yattaqillaha yaj'al lahu makhraja

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ فَارِقُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖ وَأَشۡهِدُواْ ذَوَيۡ عَدۡلٖ مِّنكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَ لِلَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مَخۡرَجٗا ٢

Fa idhā balaghna ajalahunna fa amsikūhunna bima'rūfin aw fāriqūhunna bima'rūfin wa ashhidū dhaway 'adlim minkum wa aqīmush-shahādata lillāhi dhālikum yū'azu bihī man kāna yu'minu billāhi wal-yawmil-ākhiri waman yattaqillāha yaj'al lahū makhrajā

Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. 2

Maelezo ya chini

2 Wakikaribia walio achwa mwisho wa eda zao warejeeni mkae nao kwa wema na ihsani, au farikianeni nao bila ya madhara. Na washuhudisheni kuwarejea na kufarikiana watu wawili waadilifu miongoni mwenu, na toeni ushahidi kwa mujibu wake kwa kumsafia Mwenyezi Mungu. Hayo mliyo amrishwa ndiyo anayo waidhiwa mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na mwenye kumkhofu Mwenyezi Mungu akazishika amri zake na akaepuka makatazo yake atamjaalia njia ya kutokana na kila dhiki.

وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَيۡءٖ قَدۡرٗا ٣

Wayarzuqhu min haythu lā yahtasibu waman yatawakkal 'alallāhi fahuwa hasbuhū innallāha bālighu amrihī qad ja'alallāhu likulli shay'in qadrā

Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake. 3

Maelezo ya chini

3 Na atamtengezea sababu za kupata riziki kwa jiha ambazo hata hazimpitikii katika fikra zake. Na mwenye kumwachia mambo yake yote Mwenyezi Mungu basi Yeye ni Mwenye kumtosha, hana haja ya mwengine. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kutimiza alitakalo, ni Mwenye kutekeleza alipendalo. Amejaalia kila kitu na wakati wake, wala haupitikii, na kipimo hakivuki.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat At-Talaq yote

Maswali

Wa man yattaqillaha yaj'al lahu makhraja iko wapi katika Qur'ani?

Wa man yattaqillaha yaj'al lahu makhraja iko katika Surat At-Talaq, 65:2-3.