Surat Sad, aya 51

38:51

مُتَّكِـِٔينَ فِيهَا يَدۡعُونَ فِيهَا بِفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ وَشَرَابٖ ٥١

Muttaki'īna fīhā yad'ūna fīhā bifākihatin kathīratin washarāb

Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji. 51

Maelezo ya chini

51 Watakuwa wamekaa humo wakiegemea juu ya makochi na vitanda kama wafanyavyo wenye taanusi, wakistarehe kwa kutaka matunda ya kila namna na vinywaji.