Surat Sad, aya 17

38:17

ٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱذۡكُرۡ عَبۡدَنَا دَاوُۥدَ ذَا ٱلۡأَيۡدِۖ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ ١٧

Isbir 'alā mā yaqūlūna wadhkur 'abdanā dāwūda dhal-aydi innahū awwāb

Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia. 17

Maelezo ya chini

17 Ewe Muhammad! Yastahamilie hayo wanayo yasema juu yako washirikina. Na mkumbuke mja wetu, Daudi, mwenye nguvu katika Dini na dunia. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kurejea kwa Mwenyezi Mungu katika hali zote.