وَثَمُودُ وَقَوۡمُ لُوطٖ وَأَصۡحَٰبُ لۡـَٔيۡكَةِۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡأَحۡزَابُ ١٣
Wathamūdu waqawmu lūtin wa ashābu l'aykati ulā'ikal-ahzāb
Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi. 13
Maelezo ya chini
13 Na kina Thamudi na Kaumu Lut'i na Kaumu ya Shuaibu, na watu wa Machakani, kwenye miti mingi iliyo shikamana. Hao ndio walio jumuika kuwapinga Mitume wao kama walivyo jumuika watu wako.