Huwallahul-ladhi

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۖ هُوَ ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلرَّحِيمُ ٢٢

Huwallāhul-ladhī lā ilāha illā huwa 'ālimul-ghaybi wash-shahādati huwar-rahmānur-rahīm

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. 22

Maelezo ya chini

22 Yeye Mwenyezi Mungu ambaye hapana wa kuabudiwa kikweli isipo kuwa Yeye peke yake, Mwenye kujua lilio pita na lilioko sasa. Yeye ndiye Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡقُدُّوسُ ٱلسَّلَٰمُ ٱلۡمُؤۡمِنُ ٱلۡمُهَيۡمِنُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡجَبَّارُ ٱلۡمُتَكَبِّرُۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ٢٣

Huwallāhul-ladhī lā ilāha illā huwal-malikul-quddūsus-salāmul-mu'minul-muhayminul-'azīzul-jabbārul-mutakabbiru subhānallāhi 'ammā yushrikūn

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo. 23

Maelezo ya chini

23 Yeye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye, Mwenye kumiliki kila kitu kwa hakika, Aliye safika na kila upungufu, Aliye takasika na kila lisio mwelekea, Mwenye kusalimika na yote ya upungufu, Mwenye kuwaamini na kuwasadiki Mitume wake aliyo wapa nguvu kwa miujiza, Mlinzi Mwenye kuangalia kila kitu, Mwenye kushinda basi hashindwi na chochote, Mkubwa wa shani katika nguvu na utawala, Mwenye kutukuka na kila kisicho kuwa laiki na uzuri wake na utukufu wake, Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.

هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡخَٰلِقُ ٱلۡبَارِئُ ٱلۡمُصَوِّرُۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ يُسَبِّحُ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ٢٤

Huwallāhul-khāliqul-bāri'ul-musawwiru lahul-asmā'ul-husnā yusabbihu lahū mā fis-samāwāti wal-ardi wahuwal-'azīzul-hakīm

Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima. 24

Maelezo ya chini

24 Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye kuviumba vitu vyote tangu mwanzo bila ya ruwaza ya kuigia iliyo tangulia, Mwenye kuvipa sura kama vilivyo kwa mujibu wa atakavyo Yeye. Yeye ndiye Mwenye Majina Mazuri, Mwenye kutakaswa na kila kisicho kuwa laiki yake na kila kilichoko katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye kushinda, asiye shindwa na kitu. Mwenye hikima katika kupanga kwake na sharia zake.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Hashr yote

Maswali

Huwallahul-ladhi iko wapi katika Qur'ani?

Huwallahul-ladhi iko katika Surat Al-Hashr, 59:22-24.