La ikraha fid-din

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

لَآ إِكۡرَاهَ فِي ٱلدِّينِۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشۡدُ مِنَ ٱلۡغَيِّۚ فَمَن يَكۡفُرۡ بِٱلطَّٰغُوتِ وَيُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسۡتَمۡسَكَ بِٱلۡعُرۡوَةِ ٱلۡوُثۡقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَاۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ٢٥٦

Lā ikrāha fid-dīni qat tabayyanar-rushdu minal-ghayyi faman yakfur bit-tāghūti wayu'mim billāhi faqadistamsaka bil-'urwatil-wuthqā lanfisāma lahā wallāhu samī'un 'alīm

Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 256

Maelezo ya chini

256 Hapana ruhusa kumlazimisha yeyote kuingia katika Dini. Kwa Aya na Ishara zilio zagaa Njia ya Haki imewekwa wazi kutokana na njia ya upotovu. Basi aliye ongoka akafuata Imani na akakataa kufuata chochote kisicho ingia akilini, na kinacho mpelekea kuacha Haki, basi huyo ameshika njia madhbuti kabisa ya kumkinga asiingie katika upotovu, kama yule mwenye kukamata kishikio imara kilicho fungika baraabara kitacho mlinda asitumbukie shimoni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua mnayo yatenda, na ni Mwenye kukulipeni kwa vitendo vyenu.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Baqarah yote

Maswali

La ikraha fid-din iko wapi katika Qur'ani?

La ikraha fid-din iko katika Surat Al-Baqarah, 2:256.