Surat Ibrahim, aya 15

14:15

وَٱسۡتَفۡتَحُواْ وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ ١٥

Wastaftahū wakhāba kullu jabbārin 'anīd

Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi. 15

Maelezo ya chini

15 Hao Mitume waliomba nusura wawashinde hao watu wao wanao wapinga, baada ya kukata tamaa kuwa hawataamini tena. Mwenyezi Mungu aliwanusuru, na wakafuzu, na akakhasiri kila mwenye kiburi, akakataa kumt'ii Mwenyezi Mungu, akawa shadidi wa upinzani. (Haya yaliyo wapata Mitume huwapata watu wa Mungu wote wanao wania Haki hata katika zama zetu. Ushindi wa mwisho daima unakuwa kwa walio wema, hoja kuvumilia na kuendelea na kazi ya Mungu).