كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّمَدۡيَنَ كَمَا بَعِدَتۡ ثَمُودُ ٩٥
Ka al lam yaghnaw fīhā alā bu'dal limadyana kamā ba'idat thamūd
Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia walivyo angamia watu wa Madyana, kama walivyo angamia watu wa Thamud! 95
Maelezo ya chini
95 Mambo yakawishia, na athari zao zikapotea. Wakawa kama kwamba hawajapata kukaa katika majumba yao! Hali yao ikatamka ya kumzindua kila mwenye akili apate kuzingatia! Zingatia basi maangamizo ya Madyana, na vipi walivyo baidika na rehema ya Mwenyezi Mungu kama walivyo baidika watu wa Thamud kabla yao!