قَالَ سَـَٔاوِيٓ إِلَىٰ جَبَلٖ يَعۡصِمُنِي مِنَ ٱلۡمَآءِۚ قَالَ لَا عَاصِمَ ٱلۡيَوۡمَ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِ إِلَّا مَن رَّحِمَۚ وَحَالَ بَيۡنَهُمَا ٱلۡمَوۡجُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُغۡرَقِينَ ٤٣
Qāla sa'āwī ilā jabalin ya'simunī minal-mā'i qāla lā 'āsimal-yawma min amrillāhi illā mar rahima wahāla baynahumal-mawju fakāna minal-mughraqīn
Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi likawatenganisha, akawa katika walio zama. 43
Maelezo ya chini
43 Mtoto hakumt'ii baba yake mwenye kumwonea huruma! Akasema: Nitakwenda pahala pa kunilinda na maji! Baba, mwenye kujua hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa wenye kuasi, alisema: Ewe mwanangu! Hakipatikani cha kuzuia hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwazamisha walio dhulumu! Basi yule kijana akapotea kwenye macho ya baba yake anaye mnasihi nyuma ya wimbi lilio panda juu; akawa pamoja na wakanushao, walio zama, walio teketea.