Surat Hud, aya 36

11:36

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤۡمِنَ مِن قَوۡمِكَ إِلَّا مَن قَدۡ ءَامَنَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ ٣٦

Wa ūhiya ilā nūhin annahū lan yu'mina min qawmika illā man qad āmana falā tabta'is bimā kānū yaf'alūn

Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa: Hataamini yeyote katika watu wako ila wale walio kwisha amini. Basi usisikitike kwa waliyo kuwa wakiyatenda. 36

Maelezo ya chini

36 Mwenyezi Mungu akamletea wahyi Nuhu akamwambia: Hatakusadiki wala hataifuata Haki yeyote katika kaumu yako baada ya sasa, isipo kuwa wale walio kwisha tangulia kukuamini kabla ya hayo. Basi ewe Nuhu! Usihuzunike kwa sababu ya waliyo kuwa wakikutendea, ya kukukadhibisha, na kukuudhi. Kwani Sisi tutawalipiza karibu.