Surat Hud, aya 37

11:37

وَٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ ٣٧

Wasna'il-fulka bi a'yuninā wawahyinā walā tukhātibnī fil-ladhīna zalamū innahum mughraqūn

Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa. 37

Maelezo ya chini

37 Tukamwambia: Tengeneza chombo chini ya uangalizi na ulinzi wetu, wala usinisemeze kwa ajili ya hawa madhaalimu, kwa sababu nilikwisha itikia ombi lako, na nimekwisha amrisha wateketezwe kwa kuzamishwa. Tazama Aya 27 Surat Al Muuminun (23).