Surat Hud, aya 19

11:19

ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ ١٩

Alladhīna yasuddūna 'an sabīlillāhi wayabghūnahā 'iwajan wahum bil-ākhirati hum kāfirūn

Ambao wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaitakia ipotoke, na wanaikataa Akhera. 19

Maelezo ya chini

19 Hawa ndio wanawageuza watu wasiifuate Dini ya Mwenyezi Mungu, na wanawazuia. Nayo hiyo ndiyo Njia yake Iliyo Nyooka. Na wanataka Njia hii iwafikiane na matamanio yao na pumbao lao, kwa hivyo yende upogo. Hao wanaikanya Akhera, na yaliyomo ndani ya kulipwa thawabu Muumini na kuadhibiwa kafiri.