Surat Hud, aya 18

11:18

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُعۡرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمۡ وَيَقُولُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ أَلَا لَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ ١٨

Waman azlamu mimmaniftarā 'alallāhi kadhiban ulā'ika yu'radūna 'alā rabbihim wayaqūlul-ashhādu hā'ulā'il-ladhīna kadhabū 'alā rabbihim alā la'natullāhi 'alaz-zālimīn

Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu, 18

Maelezo ya chini

18 Hapana walio zidi kujidhulumu nafsi zao na wakajitenga mbali na Haki kuliko wale wanao tunga uwongo, na kisha wakamnasibishia Mwenyezi Mungu. Hakika watu hawa Siku ya Kiyama watadhihirishwa mbele ya Mola wao Mlezi awahisabie kwa yale maovu waliyo yatenda. Mashahidi miongoni mwa Malaika, na Manabii, na wengineo, watasema: Hawa ndio walio tenda makosa maovu kabisa na dhulma kwa mintarafu ya Muumba wao! Hapana shaka laana ya Mwenyezi Mungu itawapata hao kwa kuwa ni wenye kudhulumu.