Surat Hud, aya 114

11:114

وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ ١١٤

Wa aqimis-salawāta tarafayin-nahāri wazulafam minal-layli innal-hasanāti yudhhibnas-sayyi'āti dhālika dhikrā lidh-dhākirīn

Na shika Swala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka. 114

Maelezo ya chini

114 Ewe Nabii! Timiza Swala kwa ukamilifu katika ncha mbili za mchana, na nyakati mbali mbali za usiku. Kwani Swala husafisha nafsi na hushinda katika kung'oa shari, na hufuta athari ya maovu ambayo mwanaadamu shida kuepukana nayo! Hayo uliyo amrishwa, ewe Nabii, katika uwongofu wa kheri ni mawaidha ya kuwanufaisha wale ambao walio tayari kuyakubali, ambao kwamba wanamkumbuka Mola wao Mlezi, wala hawamsahau.