Surat Hud, aya 105

11:105

يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ ١٠٥

Yawma ya'ti lā takallamu nafsun illā bi idhnihī faminhum shaqiyyun wasa'īd

Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kati yao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha. 105

Maelezo ya chini

105 Kikija kitisho chake mwanaadamu hatoweza kusema ila kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu. Kwani miongoni mwa watu wapo wenye mashaka, dhiki, wasio na bahati kwa kila namna ya shida watazo pata. Hao ndio makafiri. Na wengine wenye furaha, walio bahatika, kwa neema zinazo wangojea Akhera. Hao ndio Waumini.