Surat Fussilat, aya 46

41:46

مَّنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ أَسَآءَ فَعَلَيۡهَاۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّٰمٖ لِّلۡعَبِيدِ ٤٦

Mman 'amila sālihan falinafsihī waman asā'a fa'alayhā wamā rabbuka bizallāmil lil-'abīd

Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja. 46

Maelezo ya chini

46 Mwenye kutenda vitendo vyema ujira wake ataupata mwenyewe, na mwenye kutenda uovu madhambi yake yatakuwa juu yake. Na Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja wake, hata amtese mtu kwa dhambi za mwengine.