Surat Fussilat, aya 47

41:47

۞ إِلَيۡهِ يُرَدُّ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِۚ وَمَا تَخۡرُجُ مِن ثَمَرَٰتٖ مِّنۡ أَكۡمَامِهَا وَمَا تَحۡمِلُ مِنۡ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلۡمِهِۦۚ وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ أَيۡنَ شُرَكَآءِي قَالُوٓاْ ءَاذَنَّٰكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٖ ٤٧

Ilayhi yuraddu 'ilmus-sā'ati wamā takhruju min thamarātim min akmāmihā wamā tahmilu min unthā walā tada'u illā bi'ilmihī wayawma yunādīhim ayna shurakā'ī qālū ādhannāka mā minnā min shahīd

UJUZI wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayo waita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo watasema: Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo. 47

Maelezo ya chini

47 Kwa Mwenyezi Mungu peke yake ndio unarejea ujuzi wa kusimama Saa ya Kiyama. Matunda hayatoki kwenye vifuniko vyake, wala mwanamke hachukui mimba wala hazai ila awe Yeye anajua. Na kumbuka siku ambayo Mwenyezi Mungu atawaita washirikina, kwa kuwakebehi, awaambie: Wako wapi hao washirika wangu mlio kuwa mkiwaomba badala yangu? Watasema kwa kutaadhari: Ewe Mwenyezi Mungu! Tunakujuvya kuwa sisi hatuna wa kushuhudia kuwa wewe una mshirika yeyote.